Simulizi za Mapenzi

Jenni na Mathayo!

Sura ya Kwanza
Stori ya mapenzi yetu na Mathayo imeanza hata kabla hatujakutana. Na ukiifikiria, nikama mapenzi ya wengi yanavyoanza. Kila wakati yanapelekea kumpata mume au mke wa baadae, na yanakuandaa kuwa na mtu uliyepangiwa. Maumivu ya moyo yaliyopita au upweke unaweza ukawa na umuhimu katika maisha ya ndoa. Wakati mwingine tunatakiwa kujua hisia mbaya ili nzuri ikija tunakuwa na uhakika. Nilivyokuwa nina miaka 18 na nina fanyakazi katika mgahawa wa familia, nilikutana na mwanaume ambaye ana miaka 10 zaidi yangu. Ndio ambaye tulikuwa nae kabla ya Mathayo. Tulikuwa pamoja katika mahusiano kwa muda wa miaka 3 na nusu, hata tukaishi pamoja katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu wa mwisho wa mahusino.Uhusiano wetu haukuwa mbaya, alikuwa ni mwanaume mzuri na mimi msichana mzuri. Kiukweli tulipendana. Katika muda wote wa miaka mitatu na nusu, nilikuwa na hisia ndani yangu ambayo ilikuwa inaniambia kuwa huyu sio kwa ajili yangu. Pamoja na moyo wake mzuri alikosa hamu ya maendeleo, na alikuwa na matumizi mabaya ya fedha, alikuwa anaakili na mwenye mvuto lakini alikosa kujiamini kuhusu maisha yake. Nilimuelewa. Nilielewa pia familia yake ilikuwa haijajiandaa kwa maisha yake na maamuzi mabaya aliyoyafanya kama mwanaume mdogo wamemfanya kudumbukia katika shimo ambalo hawezi kujitoa mwenyewe


Jinsi miaka ilivyoendelea kwenda, ndivyo alivyoshindwa kunipa kile kidogo nilichokihitaji, mambo yakawa magumu kwetu. Nilikuwa ni msumbufu sana na ninaliona hilo sasa hivi. Lakini tatizo ni kwamba kulikuwa kuna vitu vingi kuhusu yeye ambavyo nilikuwa nataka kuvibadilisha, ndio nikagundua kuwa sitaweza kumbadilisha na siitaji. Nilihangaika sana kujua ni kitu gani sahihi kufanya kwa wakati ule, kukazidi kunimaliza usiku na mchana kwa sababu nilikuwa sipati taswira ya mimi bila yeye, na kuwa mwenyewe kulikuwa kunaniogopesha.
Wakati nipo katikati haya mambo yote, nikasoma kitabu kinaitwa The Secret (SIRI) ambacho kilikuwa kinaongelea Law of attraction (Sheria/Kanuni za Mvuto). Kiukweli kilinistajabisha kwa yale yaliyomo. Nikagundua kuwa sijayapanga maisha yangu kama ninavyotamani yawe! Sipendi kuruka hii kwa sababu ni muhimu, lakini ngoja tu niseme kwamba nilijua nilihitajika kufanya maamuzi kuhusu maisha yangu ya baadae yaweje. Nikaanza kuchukua hatua kuhusu maisha yangu mazuri ya baadae. Na uhusiano ulikuwa ni kikwazo kwa wakati ule. Nikajua katika moyo kama nikiendelea kukaa pale nilipo maisha siku zote yataendelea kuwa magumu.
Kwa hiyo siku moja ikafikia tukaachana. Tukaongea na kulia kwa masaa lakini mwishowe tukakubaliana uhusiano wetu haukuweza kufanikiwa. Akaamua kutoka na kuniacha mimi niendelee kukaa katika hiyo nyumba ndogo. Kwa mapato yake mwenyewe hasingeweza kukaa katika ile nyumba (nikaongeza meza za kutosha ili niweze kupata hela za kutosha kulipa bili).
Kiukweli ninaweza nikasema kwamba siku 2 za kwanza baada ya kuachana ndio zilikuwa mbaya kuliko zote maishani mwangu. Nililia vibaya, yale machozi ambayo yanatoka ndani ambapo huwezi kujua kama yapo, sehemu ya hofu na kujikuta upo mwenyewe kabisa.

Na hiyo ndio sehemu ambayo nilikuwa nilipokutana na Mathayo. Tulikutana baada ya siku 2 kuachana, ambapo unaweza ukawa mda mbaya sana au mda mzuri sana. Nikachagua kuamini kuwa ni muda muafaka kabisa.
Lakini ngoja turudi nyuma kwa dakika moja, kumbuka nilivyokuwa nafanya kazi katika mgahawa, kwa miaka mingi nilikuwa nasubiria kukutana na wakwe zangu bila kujua. Ngoja tuwaite Mr. and Mrs D.
Walikuwa ni watu wa kawaida tu, Mrs. D  alikuwa ni mzuri na rafiki kwa watu na Mr. D alikuwa ni mtaratibu na mgumu kumsoma. Nilikuwa nafurahi kuwasubiria, nilikuwa naona furaha sana wakati Mrs. D akimuongelea mtoto wao mpendwa aliye mbali ambaye alikuwa anasema tungependeza sana katika mahusiano. Tulikuwa tunacheka lakini nikawa namkumbusha kwamba nina mpenzi. Nikaja nikajua baadae Mrs. D wakati mwingi alikuwa anamuongelea Mathayo na mimi. Mr. D akasema ilimbidi asikilize kila kitu wakati wakija katika mgahawa, na Mathayo alipokuja kwa nyakati tofauti alisikia kuhusu mimi, lakini kwa sababu tofauti sikuwepo wakati walipokuja, hatukuweza kukutana.

Lakini siku moja, Januari tarehe 19, 2009, tulikutana. Lakini cha kushangaza nilikuwa hata sifanyi kazi siku hiyo! Kiukweli kukutana kulikuwa kwa bahati.
Nikajua kidogo nilivyoamka asubuhi maisha yangu yalikuwa yanataka kubadilika juu chini.




Sura ya Pili
Ilikuwa jumamosi mimi na mpenzi wangu wa zamani tulipoachana, ilipofika jumatatu asubuhi nilikuwa najisikia mwenye matumaini kidogo na kufikiria kupata chai na rafiki. Mwanaume mmoja ambaye kama kaka yangu ambaye tulikuwa tunafanya nae kazi pamoja kwa muda wa miaka sita na nusu mpaka kipindi hichi cha stori, yeye na mimi tumekuwa karibu mpaka tukawa tupanga kunywa chai pamoja na kuongelea matukio katika maisha yetu. Kabla ya wiki moja ya hii jumatatu yeye na mimi tulielewana tukutane pale kupata chai, ikatokea nikaitwa kazini kwa sababu mfanyakazi mmoja alikuwa anaumwa. Nilikuwa sijui kwa wakati ule, kumbe ningekutana na rafiki yangu siku ile nisingepata kuonana na Mathayo. Maisha yangu yangekuwa tofauti sana sasa hivi. Inafurahisha maamuzi madogo katika maisha yanaweza kubadilisha maisha yetu yote.
Siku hii ya jumatatu  niliamka asubuhi, nikaoga na kuvaa, nikatoa muda wa saa 3 asubuhi kuelekea kupata chai na rafiki yangu. Kama kawaida nilikuwa nimechelewa dakika chache. Nilipofika nikaenda katika sehemu ambayo rafiki yangu alikuwa anasubiria. Tukaongea kama sekunde thelathini mara mlango wa mgahawa ukafunguliwa, kwa mshangao alikuwa ni Mrs. D! alikuwa na furaha mara baada ya kuniona, akaniambia “Jenni, najua hii sio kawaida na ninajua una mpenzi, lakini mtoto wangu amekuja na sisi ndio tunaondoka ndio nikakuona umekuja, ningependa uje nje ukutane nae!”
Nikamkumbatia halafu tukacheka, nikisema hata hivyo mimi na mpenzi wangu tumeachana kwa hiyo hamna tatizo. Mrs. D akaniongoza njia nje alipokuwa anasubiri, nikakuta mlango wa gari wa pembeni upo wazi wakati anatoka. Nikaingiza kichwa kwenye gari ndio nikamuona mtoto wao mwenye sifa mbaya.

Nitadanganya kama nisiposema kwamba niliwasikia malaika wakiimba au ninaweza nikasema kwamba mwanga wa kung’aa katika yeye kama vile ametoka kwa Mungu. Lakini kiukweli alikuwa ni wa kuvutia. Akatoka katika siti ya abiria na kuja kunisalimia kwa kunishika mkono, akisema “ni vizuri hatimaye tumekutana!”
Alikuwa na macho mazuri ambayo sijawahi kuyaona na kuanzia hapo nilikuwa nimepigwa na bumbuwazi, ambapo sio kawaida yangu ninapokubwa na mazungumzo enye kufedheha ya kijamii (sanasana inayonikutanisha na watu wa jinsia tofauti ambao wanavutia)
Nikasema kitu katikati “nafurahi sana kukutana na wewe pia! Nimesikia vitu vingi sana kuhusu wewe na ninampenda mama yako!”
Mrs. D akasema Mathayo anaenda nyumbani halafu asubuhi yake anaondoka lakini atarudi baada ya wiki chache. Nikasema labda tutaonana tena akirudi, na maongezi yakaisha kwa furaha.
Lakini Jenni mwenyewe asili, nikaona angalau niseme kitu kimoja cha mzaha kabla siondoka na furaha yangu! Nikageuka nikaingiza kichwa kwa mara ya pili kwenye gari nikasema, “samahani mheshimiwa? Hivi ulisema unaitwa nani? Nimeshasahau!” nimemuita mheshimiwa? Nilipolitaja tu hilo neno nikawa motifu na mimi mwenyewe. Nimemuita mheshimiwa??? Mjinga gani mimi!!
Akacheka akasema “Mathayo.”
“Haya asante! Nikasema, “labda nitakuona hivi karibuni!”
Wakaondoka, nikarudi kule kwenye Hoteli ambapo rafiki yangu alikuwa ananisubiri!. Na baad ya dakika chache tulikuwa ndani tulikuwa ndani tumekaa katika meza yetu. Tukaagiza chai na baada ya dakika chache mhudumu akaja na kikaratasi kimeandikwa akaniambia “yule jamaa amerudi amesema hataki kukusumbua kwa sababu umekaa na Chris.” Moyo ukapiga kidogo, nikafungua kile kikatasi. Mathayo ameandika jina lake na namba yake ya simu na ujumbe: Ntarudi baada ya wiki mbili, ntafurahi kusikia kutoka kwako! Nilikuwa natetemeka siwezi sema kwanini, lakini nilikuwa kama naota! Akili yangu ilikuwa inakimbia kuhusiana na hili tukio, lakini sikajisikia vibaya kuendekeza mawazo ya uhusiano mpya wakati ule mwingine umeisha hivi karibuni.
Mmoja ya wahudumu katika hoteli yetu ambaye ni rafiki yangu ambaye kama mama, akaja katika meza yetu akasoma kikaratasi, na Mathayo alivyokuja ndani akawa ananiangalia kwa nyuma wakati ninaongea na rafiki yangu. Kwa muangalio huo wa sura yake akasema “Jenni, hili ni suala la Mungu.”
Kusema kweli alikuwa yupo sawa!

Mrs. D na Mathayo wote wakaanza kuniongelea baada ya kukutana mara ya kwanza, Mathayo akamwambia mama yake mimi ndiye amenichagua, na kwamba alijua tu na mama yake akasema na mimi nilijua tu. Akamwambia nilichomwambia kuhusu kuachana na mpenzi wangu na Mathayo akadai warudi. Walivyorudi akaandika maneno katika kipande cha karatasi na akaja kunitafuta.



Sura ya Tatu
Zikapita siku tatu baada ya kukutana, na ile karatasi aliyoniandikia ikabaki katika mkoba wangu! Nilikuwa sifati kabisa kanuni zozote za siku ngapi kusubiri kabla kupiga simu; lakini nilikuwa najisikia vibaya kutompigia simu kabisa, ukizingatia mimi mwenyewe sina mpenzi. Mpenzi wangu wa zamani bado hata hajahama katika ile nyumba tuliopanga, lakini nikaendelea kujua uwepo wa ile karatasi na ninataka kumpigia simu kisirisiri, nikashindwa. Nikawa naona kama ni makosa kuwa na mawazo ya mpenzi mwingine karibuni tu!
Wakati wa mchana katika siku ya nne, nilienda kazini na wakati naandika katika daftari la kuingia kazini, nikaona kijiti na kikatasi kimeviringishwa dirishani kikiwa kimeandikwa jina langu. Nikakifungua na kilikuwa kimeandikwa Mathayo na nambaa yake ya simu tena, lakini wakati huu ulikuwa muandiko wa mhudumu aliye pokea simu.
Nikaenda kwa Meneja nikamuuliza hii ni nini tena, Huyu jamaa ameshanipa namba yake! Hichi kikaratasi kinatafuta nini hapa?
Meneja wangu akaniambia kwa makwarukaru kwamba Mathayo amepiga simu katika hoteli na kuniulizia mimi, kwa vile sikuwepo akaacha namba yake na jina lake kwa mhudumu. Huyu bwana anakusumbua? Unataka nimpigie simu? Akauliza kwa kujali.
Nikacheka na nikasema sikufikiria hivyo. Lakini kimoyomoyo nilishangazwa na nguvu ya kung’ang’ania ya  Mathayo. Alikuwa amenipenda lakini alikuwa anazunguka kuniambia. niliipenda hiyo
Nilimtumia ujumbe hiyo mchana na nikaomba samahani kwa kutopiga simu. Nikamwambia kwamba ningependa lakini ni siku chache tu ntangu tumeachana na mpenzi wangu wa zamani. Kwa hiyo nikawa sijisikii vizuri kumpigia mwanaume mwingine karibuni tu! Nikamwambia ntampigia usiku baada ya kutoka kazini.
Majibu ya ujumbe yalikuwa hivi “ Sawa, Miss wa siku nne! Kitu kizuri nimeendelea kuwa na matumaini, kwa sababu nilianza kuona kama sitasikia kutoka kwako!”
Mathayo baadae aliniambia, zile zilikuwa siku nne zenye mateso kuliko zote maishani mwake. Aliweka simu yake karibu na kutafakari kama nilikuwa nakuwa mgumu kupata au kitu kingine. Wakati hakupata mawasiliano toka kwangu, alipiga simu kwenye hoteli, ikitokea nimepoteza namba yake! Si mtu wa uvumilivu! Ninaweza nikajaribu hata hilo sasa!
Sitaki kuengua kitu chochote, lakini pia sitaki kuyaongelea haya mambo kwa kila wiki. Basi hebu tuseme kwamba nilimpigia simu Mathayo ile usiku, tukamaliza mazungumzo ya kama saa moja. Nilijua kwamba ndio tu nimekutana naye, mwanaume ambaye siku moja atakuwa mume wangu. Siku iliyofuata nikampigia simu rafiki wangu wa karibu nikamwambia hivyo, ambayo, kwa kawaida, alikuwa na kiasi fulani cha wasiwasi. Akaguna akasema sawa!



Ukweli ni kwamba, uhusiano wangu na rafiki na familia ulikuwa sio mzuri, kila kitu kilitokea kwa haraka, baada tu ya muda mfupi wa mahusiano ya yaliyopita.
Mathayo alikuwa na miaka saba zaidi yangu, alikuwa na kazi yenye mafanikio katika bima na huduma za kifedha, aliishi mbali, lakini alionekana amekufa juu yangu. Watu hawakumwamini, na hata na mimi nilikuwa na shaka kwa mambo yalivyokuwa na kasi kama ya umeme.
Wakati wa wiki baada ya kuongea na simu mara ya kwanza, tulikuwa tunaongea kwa masaa kila usiku. Nikajifunza kwamba alikuwa ni mshabiki mkubwa wa kitabu cha Siri, kama mimi nilivyokuwa, akasema “anataka kuishi maisha yeye yampendezayo!” Kukutana kwetu ni bahati? Sidhani.
Pia aliniambia kuwa amerudisha nyuma safari yake ili aweze kupata muda mwingi wa kukaa na mimi, tulikuwa ya kwanza kukutana tulikuwa tumeshapanga chini ya wiki mbili baada ya kukutana. Nakumbuka kupata maandishi kutoka kwake siku chache kabla ya kuondoka kuwa “hakuweza kusubiri mimi kuwa katika mikono yake” Nilipata wasiwasi kidogo kutokana na hili, kutokana na kwamba tarehe yetu ya kwanza ya kukutana bado. Lakini niliipenda hiyo yote. Nilijisikia vizuri kuwa na mtu anaekutaka bila kuwa pazia la kujifanya na tahadhari, tabia inayokubalika. Mathayo ni mmoja ya watu wachache hapa duniani ambao wanajitupa katika uhusiano bila ya kuwa na aibu na bila kusita kwa kila watakacho kitaka.
Hivyo  tarehe yetu ya kwanza kukutana, mimi nilivaa vazi jeusi kidogo na sweta la kijani linalong’aa na yeye alivaa jinsi na shati yenye vifungo vyeusi. Tulikutana sehemu inayoitwa Starbucks, tulikumbatiana kama marafiki wa zamani, akanipeleka kwenye gari aliloazima kutoka kwa baba yake, akanifungulia mlango kama muungwana wa ukweli. Akawasha gari na akaweka CD kucheza nyimbo ambazo huwa nazipenda, moja baada ya nyingine. Nilimuuliza akasema ametoa katika akaunti yangu ya facebook nyimbo ambazo nimeziandika nazipenda, lakini alikataa siku hiyo kuniambia. Aidha alikuwa anadanganya au tulikuwa tunapenda aina moja ya miziki. Njia yoyote tulikuwa kamilifu.
Na jioni ikaanza wiki ya kwanza tulivyokutana, tulipata chakula cha usiku mara kadhaa, tukaenda sinema kuangalia filamu, tukasherehekea siku yake ya kuzaliwa na babu na bibi yake na wazazi wake, na kisha alisema kwaheri yenye uchungu sana kabla hajaondoka kurudi kazini.
Nadhani ilikuwa ni siku ya tatu katika wiki ile ndio nilianza kumpenda kiukweli. Tulikuwa kina chini ya ardhi katika mapango na kumsikiliza mwongozaji msafara ambavyo alikuwa anatuelezea, wakati Mathayo amenishika na mikono yake kutoka nyuma na kunishika wakati tumesimama . Sina uwezo wakuelezea lakini nilijisikia nipo sawa!
Siku chache baada ya Mathayo kuondoka, katika siku ya wapendanao 2009, nilipata zawadi ya kipekee wakati nilikuwa nipo kazini, zawadi ambayo ilikuwa nzuri kuliko zote ambazo nimeshapewa ya kimapenzi.



Subiri sura ya nne hivi karibuni!

No comments:

Post a Comment